Wednesday , 17th Jun , 2015

Msanii wa muziki Dullayo ameeleza kuwa, mabadiliko makubwa ambayo yametokea katika muziki kwa sasa, ndio sababu pekee ambayo imeyumbisha nyota yake na kuonekana kuwa hafanyi vizuri kama kipindi cha nyuma.

Dullayo

Dullayo amekazia kuwa, muziki walikuwa wanafanya katika kipindi cha nyuma ndio ulikuwa muziki halisi na utaendelea kudumu, binafsi kwa upande wake akiendelea kupambana na changamoto ya mabadiliko haya ili kurejea katika chati.