
Kikosi cha Yanga
Mchezo huo ulikuwa maalumu kwa timu hizo kuonesha mchango wao kwa serikali katika jitihada za kupambana na ujangili na mauwaji ya tembo nchini, lakini pia kujiandaa na ligi kuu Tanzania bara inayotarajia kurejea wiki ijayo.
Kipindi cha kwanza kilimalizika kwa sare tasa ya bila kufungana kabla ya Yanga kujipatia bao lake dakika ya 84 kupitia kwa Yussuph Mhilu.
Katika mchezo huo, Yanga ilichezesha wachezaji wengi wa kikosi cha pili pamoja na wachezaji kadhaa wa kikosi cha kwanza akiwemo, Deus Kaseke, Heritier Makambo, Pius Buswita, Mrisho Ngassa na Raphael Daud.
Wachezaji waliokosekana katika mchezo huo ni kutokana na majukumu ya kuitumikia timu ya taifa, ambapo Juma Mahadhi na Kelvin Yondani walijumuishwa katika kikosi cha Taifa Stars kilichocheza na Uganda kwenye mchezo wa kufuzu AFCON na kutoka sare ya 0-0.