Saturday , 21st Apr , 2018

Droo ya kupanga makundi ya Kombe la Shirikisho Barani Africa inatarajiwa kufanya leo mchana jijini Cairo Misri, ambapo tayari timu ambazo zinauwezekano wa kuwa kundi moja na Yanga zikiwa zimewekwa kwenye kapu la kwanza.

Kapu la kwanza lina timu za 
1-USM Alger (Algeria)
2-Al Hilal (Sudan)
3-AS Vita Club (DRC)
4-Enyimba (Nigeria)

Kapu la pili lina timu za
1-Asec Mimosas (Ivory Coast), 
2-Yanga Sc (Tanzania)
3-CARA Brazaville (Congo)
4-Williamsville (Ivory Coast)
5-Al Masry (Egypt)
6-Aduana Stars (Ghana)
7-Gor Mahia (Kenya)
8-Djoliba (Mali)
9-Raja Casablanca (Morocco)
10-RS Berkane (Morocco)
11-UD Songo (Mozambique)
12-Rayon Sports (Rwanda)

Kwa mujibu wa kanuni za mashindano timu nne zilizopo kwenye Kapu la 1 haziwezi kukutana kwenye makundi huku timu 12 za Kapu la 2, timu 3 zinakuwa kwenye kundi moja.

Kila timu kwenye kundi itacheza mechi 6 ikiwa mechi 3 nyumbani na mechi 3 ugenini. Mechi za makundi zinatarajiwa kuchezwa kuanzia Mei 4 na 6 mpaka Agosti 28 na 29.