
Mkuu wa Kitengo cha habari cha Yanga, Jerry Muro amesema wako katika maandalizi ya mwisho kwa ajili ya kutafuta mechi za kirafiki ambazo zitawasaidia kuwaweka vizuri zaidi kwani michuano hiyo ni migumu hivyo maandalizi ya nguvu ni muhimu.
Muro amesema, Lengo la Yanga ni kupata mechi kadhaa za kirafiki ili kujiweka fiti zaidi na kocha Hans Van Der Pluijm atapata muda wa kutosha wa maandalizi ikiwa ni pamoja na kuangalia mapungufu ya kikosi na mchezaji mmoja mmoja ili kufanyia marekebisho.
Kambi ya Yanga inatarajia kuwa katika mji wa Johannesburg ambako itaweka kambi inayotarajiwa kuwa ya zaidi ya siku tano.