Wednesday , 18th Feb , 2015

Michuano ya ligi kuu soka Tanzania Bara inaendelea kesho (Februari 19) kwa timu ya Yanga kuwa wenyeji wa Timu ya Tanzania Prisons mechi itakayochezwa Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Kwa upande wa pili wa michuano hiyo, Mabingwa watetezi wa Kombe hilo, Timu ya Azam Fc itaikaribisha Ruvu Shooting Uwanja wa Chamazi jijini Dar es salaam.

Katika muendelezo wa Ligi hiyo, Yanga itakutana na Mbeya City ya jijini Mbeya mechi itakayopigwa mwishoni mwa juma hili.

Msemaji wa Mbeya City, Dismas Ten amesema, baada ya kulazimishwa sare katika mchezo uliopita dhidi ya Coastal Union jijini Tanga, sasa hasira zao wamezielekeza kwa Yanga.

Ten amesema, Licha ya Yanga kupata ushindi dhidi ya BDF, wanaamini watawafunga na wasitarajie kuondoka na Pointi hata moja.