Wednesday , 13th May , 2015

Timu ya taifa ya mpira wa wavu wa ufukweni ya wanawake imepoteza sifa ya kushiriki michuano ya Afrika mwaka huu na Olimpiki ya 2016 baada ya kushindwa kusonga mbele hatua ya pili mashindano ya kanda ya tano.

Akizungumza na East Africa Radio, mwenyekiti wa chama cha mpira wa wavu nchini TAVA, Muharame Mchume amesema, timu hizo zimeshindwa kushiriki mashindano makubwa ya kimataifa hivyo Tanzania haitakuwa na mwakilishi kwenye mchezo wa wavu katika michuano ya Afrika itakayofanyika Septemba mwaka huu, Congo Brazzavillle.

Mchume amesema, kutokana na matokeo hayo, wanachokifanya sasa ni kujiimarisha zaidi katika mashindano ya ndani pamoja na kutafuta michuano ya mualiko ya kimataifa katika mataifa mbalimbali ili kutafuta uzoefu wa kushindana na kuhimili mikiki mikiki ya kimataifa.