Friday , 7th Mar , 2014

Wang’amuzi vipaji 28 wanakutana Lushoto mkoani Tanga kwa siku saba katika mpango maalumu wa maboresho ya Taifa Stars ambapo watatoka na orodha ya mwisho ya wachezaji waliopatikana katika mechi za maboresho hayo zilizochezwa nchi nzima.

Afisa habari wa TFF Boniface Wambura amesema kuwa katika kikao hicho, wang’amuzi hao watapitia majina ya wachezaji walioteuliwa ikiwemo kuwaangalia tena kwenye video kwa vile mechi zote zilirekodiwa. Wachezaji watakaoteuliwa katika mpango huo baadaye wataingia kambini mkoani Mbeya.

Wang’amuzi vipaji ambao wanaoondoka Machi 9 mwaka huu kwenda Lushoto.