Wednesday , 1st Jun , 2016

Mwanariadha mkongwe nchini ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki nchini (TOC) Filbert Bayi amewataka, wanariadha wengi chipukizi wa kitanzania wasihitaji matokeo ya haraka katika medani za kimataifa ili kuweza kulinda vipaji vyao.

Bayi amesema, kizazi cha wanariadha kuanzia miaka ya 2,000 kimekuwa an haraka ya ya mafanikio kiasi cha kujikuta kikishindwa kufanya maandalizi yasiyokidhi viwango.

Bayi amesema, miaka ya nyuma walikuwa wakipata nafasi ya kushiriki michuano mikubwa ya riadha lazima wawe wameweka kambi si chini ya miezi sita ambapo kocha pamoja na meneja wakihakikisha umeshaelewa mafunzo na kuhakikisha uwezo wako wanakupeleka kushiriki tofauti na miaka ya sasa ambapo wengi hutumia mashindano ya riadha kama biashara.

Bayi amesema, miaka ya sasa mwanariadha anakuwa na mazoezi ya wiki mbili anakwenda kushiriki mashindano makubwa na katika mwaka ameshakimbia kimataifa zaidi ya mara tano huku akili yake ikiwaza kushiriki kwa ajili ya kupata pesa pasipo kujali ubora wake.

Bayi amesema, wanariadha wa hapa nchini wanamaandalizi madogo sana ambapo kwa ndani ya mwaka anashiriki mashindano matano huku akiwa na kambi ya mwezi mmoja jambo ambalo linachangia kwa kiasi kikubwa kushusha kiwango cha riadha hao nchini.

Bayi amesema, ipo haja ya wanariadha na mameneja wao kubadilika ili kufikia mafanikio aliyowahi kuvuna enzi zake.