Saturday , 30th Jul , 2016

Baraza la Michezo nchini BMT limewataka wadau wa mchezo wa Judo kuendelea kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu za ugombea wa nafasi mbalimbali za uongozi katika chama cha Judo Tanzania JATA.

Afisa habari wa BMT Halima Bushiri amesema, mpaka sasa ni wagombea wanne pekee waliojitokeza kuchukua fomu hizo ambazo zimeanza kutolewa tangu Juni 31 mwaka huu.

Halima amesema, wadau wa mchezo huo wanatakiwa kuendelea kujitokeza kwa ajili ya kuongeza idadi ya wagombea wa uchaguzi ndani ya chama hicho ambao watawania nafasi mbalimbali ambazo zipo ndani ya chama hicho.

Halima amesema, wanaamini viongozi watakaopatikana ndani ya chama hicho watasaidia kuendeleza mchezo huo hapa nchini.