Monday , 21st Dec , 2015

Kocha mkuu wa klabu ya Tanzania Prisons Salum Mayanga amesema kupoteza kwa hali ya kujiamini kwa wachezaji wake ndiko kunakopelekea timu yake kupata matokeo mabaya kwenye mechi za ligi kuu ya soka tanzania bara hivi karibuni.

kocha wa Tanzania Prisons kabla hajatua klabuni hapo akiwa kama kocha msaidizi wa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars.

Akizungumza na East Africa Radio Mayanga ameyasema hayo siku chache baada ya timu yake kupokea kipigo cha bao 4-1 kutoka kwa Jkt Ruvu kabla ya kulazimishwa sare tasa na wakatamiwa wa Mtibwa Sugar jumamosi iliyopita kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine Jijini Mbeya.

Mayanga amekiri kuwa Mtibwa wako vizuri zaidi yao kiufundi lakini vijana wake wamepunguza makosa waliyoyafanya kwenye mechi dhidi ya Jkt Ruvu lakini ameahidi kuendelea kufanya marekebisho zaidi ili waanze kupata matokeo ili kurejesha imani kwa mashabiki wake.

Tanzania Prisons inashika nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara katika mechi 12 walizocheza huku ikijikusanyia pointi 18 .