
Katibu mkuu wa shirikisho la mpira wa kikapu Tanzania TBF Saleh Zonga amesema kuwa maandalizi na mipango yote imekamilika na kinachosubiriwa ni kuanza kwa michuano hiyo mikubwa kwa ngazi ya klabu hapa nchini ambayo itakua ikifanyika katika uwanja wa ndani wa taifa jijini Dar es salaam
Aidha Zonga amesema kuwa pamoja kukosa udhamini wao kama shirikisho wamejipanga kuhakikisha mashindano yanakwenda kama yalivyopangwa na amepongeza idadi kubwa ya vilabu vilivyothibitisha ushiriki huo.
