
Venus Williams
Williams, mwenye umri wa miaka 36, alishinda kwa seti 6-4 7-6 (7-3), na sasa anakwenda kukutana na Coco Vandeweghe, aliyemchapa Garbine Muguruza wa Hispania kwa seti 6-4 6-0.
Venus amesema ana ari kubwa ya kushindana kwenye kila mechi, na angependa afike fainali na kutwaa taji hilo, kwa mara ya kwanza.
Mdogo wa Venus, Serena naye anatarajiwa kucheza mchezo wa robo fainali dhidi ya Muingereza Johanna Konta kesho Jumatano asubuhi.