Thursday , 2nd Jun , 2016

Beki mpya wa Yanga Hassan Kessy amesema hana maana ya kuendelea kupumzika huku akijua kabisa ushindani mkali ulio katika kikosi cha Yanga.

Kessy amesema ushindani ni mkubwa ndiyo maana ameamua kuendelea na mazoezi hata katika kipindi hiki cha mapumziko ili akiingia kambini awe tayari kwa ushindani.

Kessy mesema, anafurahia ushindani kwa kuwa humfanya mtu kuwa imara hivyo yuko tayari na kuisaidia timu yake.

Kessy amejiunga na Yanga akitokea Simba ambako mkataba wake umeshamalizika.