Akizungumza na East Africa Radio Afisa habari wa BMT, Najaha Bakari amesema wamepata wagombea 16 ambapo Agosti 28 watafanyiwa usaili kwa waliochukua fomu huku uchaguzi ukitarajiwa kufanyika Agosti 29 mwaka huu Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Najaha amesema wadau wa mchezo huo na wapiga kura wanatakiwa kujitokeza kujitokeza kupiga kura kwa ajili ya kupata viongozi ambao watauendeleza mchezo huo hapa nchini huku nafasi ambazo zimekosa wagombea ampaka sasa ni Makamu Mwenyekiti na muweka hazina huku nafasi ya kamishna wa ufukweni na kamishna wa njia za ufundishaji pia zikikosa watu




