
Afisa habari wa TFF Boniface Wambura amesema kuwa wameshakamilisha kila kitu kuhusiaan na kocha huyo ambaye hakumweka wazi jina lake wala anakotoka, na kinachosubiriwa ni ujio wake tu
Kwa siku za hivi karibuni tangu TFF ilipositisha kibarua cha kocha mdenmaki Kim Palsen kumekua na taarifa tofauti juu ya kocha gani ambaye atapokea mikoba ya mdenmaki huyo ambapo kwa sasa kumekua na tetesi za kocha mholanzi wa St. George ya Ethiopia uhenda akawa akatwaa nafasi hiyo.
