
Mkutano mkuu wa uchaguzi wa viongozi wa timu ya soka ya Simba unataraji kufanyika may 4 mwaka huu,
Tarehe yakufanyika uchaguzi huo imetangazwa hii leo na mwenyekiti wa klabu hiyo Ismail Aden Rage wakati akitoa ufafanuzi juu ya malipo ya usajili wa mshambuliaji wa zamani wa timu hiyo Emmanuel Okwi kwenda Etoil du Sahel ya Tunisia
Rage amesisitiza kuwa hawajalipwa pesa hizo zaidi ya milioni 480 na uthibitisho wa hilo ni Barua toka FIFA ambayo aliionyesha mbele ya waandishi wa habari huku pia Rage akiahidi kukabidhi fedha hizo na akaunti ya klabu yenye fedha nyingine zaidi ya milioni mia mbili kwa uongozi mpya utakaochaguliwa may 4 mwaka huu.
