Thursday , 10th Nov , 2016

Kikosi cha Timu ya Taifa ya wanawake Twiga Stars kinatarajiwa kucheza michezo miwili ya kirafiki dhidi ya Cameroon ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya timu ya Taifa ya Cameroon kuelekea katika Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawwake

Twiga Stars

Afisa habari wa Shirikisho la Soka nchini TFF, Alfred Lucas amesema, hapo awali Cameroon waliomba mchezo mmoja lakini wameomba kuchezwa michezo miwili ambapo wamekubaliana nao kwani wanaamini michezo hiyo itakuwa ni kipimo kizuri kwa Twiga Stars kwa ajili ya michuano mbalimbali iliyo mbele yao.

Lucas amesema, mchezo wa kwanza dhidi ya Cameroon utapigwa hapo kesho huku mchezo wa pili ukitarajiwa kupigwa Novemba 13 mwaka huu.

Kikosi cha Twiga Stars ambacho kimewasili jana nchini Cameroon ni

Makipa:

Fatma Omari na Najiat Abbas

 

Mabeki :

Wema Richard, Sophia Mwasikili, Anastasia Katunzi, Maimuna Hamisi, Fatuma Issa, Happiness Mwaipaja na Mary Masatu

 

Viungo :

Donisia Minja, Stumai Abdallah, Amina Ally, Anna Mwaisura na Fadila Kigarawa

 

Washambuliaji:

Fatuma Swalehe, Asha Rashid na Mwanahamisi Omari