Wednesday , 15th Jun , 2016

Jamii imeombwa kujitokeza kwa ajili ya kuweza kuwawezesha vijana wenye vipaji ili kuweza kupata vijana watakaoitangaza nchi katika ramani ya michezo hapa nchini.

Mkurugenzi wa kituo cha kuendeleza soka la vijana Shaban Kiemba amesema, vijana wake wamealikwa katika mashindano ya vijana ya Rolling Stone ya Afrika Mashariki na kati yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi June 29 mpaka Julai 07 mwaka huu.

Kiemba amesema, vijana hao wanauwezo wa kufanya vizuri zaidi katika miaka ya baadaye kwani michezo huanziia kwa mtoto akiwa na umri mdogo na kwa kuwezesha hivyo jamii inatakiwa kuangalia michezo kwa vijana.

Kiemba amesema, wachezaji wengi wanaofanya vizuri ni kutokana na kuinuliwa wakiwa wadogo na kwa sasa wanaleta maendeleo katika michezo hivyo kama jamii itazingatia michezo kwa vijana hao nchi itaweza kuwa na vijana ambao itaweza kurudisha heshima ya michezo hapa nchini.