Monday , 30th May , 2016

Straika wa Yanga, Mzimbabwe, Donald Ngoma, amesema haifahamu sana TP Mazembe ya DRC Congo lakini watakapokutana nayo watahakikisha wanaifunga timu hiyo ili kusonga mbele zaidi katika mashindano hayo.

Straika wa Yanga, Mzimbabwe, Donald Ngoma.

Donald Ngoma amesema haya baada ya Yanga kupangiwa kucheza na TP Mazembe ambao wapo kwenye kundi moja katika Kombe la Shirikisho Afrika.
“Siwafahamu Mazembe kwa kiasi kikubwa lakini shida yetu ni kupata matokeo mazuri yenye faida kwetu, tutapambana na lengo letu ni ushindi tu, kuwafunga itakuwa matokeo mazuri zaidi kwetu, kwa hiyo kilichopo ni kutafuta ushindi tu,” alisema Ngoma

Yanga inatarajia kuikaribisha Mazembe kati ya Juni 28 au 29 katika mchezo wa nyumbani kabla ya kurudiana huko DR Congo kati ya Agosti 23 au 24, mwaka huu.