Monday , 28th Dec , 2015

Uongozi wa Chama cha kuogelea Tanzania TSA umepanga kuanza haraka maandalizi ya michuano ya Kimataifa ya Afrika CANA kanda ya tatu itakayofanyika mwaka 2017 jijini Dar es salaam.

Katibu mkuu wa TSA Ramadhan Namkoveka amesema, wanajukumu la kuhakikisha wanaandaa timu yenye ushindani ili kupata matokeo mazuri katika michuano hiyo ambapo Tanzania watakuwa nchi wenyeji.

Namkoveka amesema, kupewa jukumu la uenyeji wa michuano ni heshima kubwa kwa Taifa hivyo haitapendeza kuona michuano hiyo ikimalizika pasipo kuchukua medali, kikombe au tuzo yoyote.

Tanzania imepewa jukumu la kuandaa michuano hiyo Desemba 13 mwaka huu katika kikao cha nchi wanachama wa kanda hiyo kilichofanyika Kampala nchini Uganda.

Tanzania ilifanikiwa kushinda medali 10 za dhahabu fedha 19 na shaba sita katika michuano iliyopita.