Monday , 22nd Dec , 2014

Kocha wa Timu ya vijana ya Kinondoni Mwenyemali Tambaza amesema mashindano ya Taifa ya vijana yataweza kusaidia vijana kuweza kufanya vizuri katika michuano mbalimbali na kuweza kupata timu nzuri ya Taifa ya Vijana.

Akizungumza na East Africa Radio, Tambaza amesema mpaka sasa ana vijana 16 ambao wanajiandaa na michuano hiyo inayotarajiwa kufanyika Desemba 30 mwaka huu jijini Mwanza kwa kushirikisha timu mbalimbali kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini.

Tambaza amesema michuano hiyo itawawezesha vijana wengi kuendelea kujiunga katika timu za vijana kutokana na Shirikisho la Soka Nchini TFF kuanzisha michuano hiyo itakayoleta mafanikio kwa vijana na Taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake Nahodha wa timu hiyo, Jose Katunzi amesema anaamini mazoezi wanayoendelea kufanya yatawasaidia kuweza kuibuka na ushindi katika michuano hiyo ya vijana.