Katibu wa Chama cha kuogelea nchini TSA Ramadhan Namkoveka amesema, mashindano hayo ni sehemu ya kutafuta viwango kwa ajili ya kufuzu kuelekea michuano ya Olimpiki itakayofanyika Septemba mwaka huu nchini Brazili.
Namkoveka amesema, iwapo timu hiyo haitafanikiwa kupata viwango vya kuweza kufuzu Olimpiki watatafuta mashindano mengine ili kuweza kupata viwango kabla ya Julai mbili mwaka huu ambayo ni siku iliyopangwa kuwa ya mwisho wa kushiriki mashindano ya kuwania kufuzu Olimpiki.