Tuesday , 8th Apr , 2014

Shirikisho la soka Tanzania TFF limebariki maamuzi ya kamati yake ya Nidhamu ya kuipa ushindi Stand United ya Shinyanga dhidi ya JKT Kanembwa baada ya Kanembwa kuchezesha wachezaji wasiostahili kwenye mechi yao ya kiporo ya Ligi Daraja la Kwanza.

Afisa Habari wa TFF Boniface Wambura

TFF imesema imeafiki maamuzi ya kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) yakuipa ushindi Stand United dhidi ya JKT Kanembwa baada ya timu hiyo kuchezesha wachezaji waliosajiliwa dirisha dogo kwenye mechi yao ya kiporo ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL).

Afisa habari wa TFF Boniface Wambura amesema uamuzi huo ulizingatia sheria na kanuni na JKT Kanembwa walikua wanajua juu ya zuio la kutowatumia wachezaji ambao hawakucheza mchezo wa awali ambao ulivunjika.