
Moja kati ya pambano la Simba na Yanga
Gharama ya viingilio vya mchezo huo vimetangazwa kwenye mkutano na wanahabari katika makao makuu ya shirikisho hilo, Karume, Ilala jijini Dar es Salaam.
VIP A, itagharimu Sh 30,000, huku VIP B na C ikiwa na thamani ya Sh 20,000 pamoja na siti za rangi ya machungwa, Bluu na Kijani ambazo ni za mzunguko zikiwa na gharama ya Sh 7,000.
Mchezo huo unatarajia kupigwa 30, Septemba katika uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam ambapo utakuwa ni mchezo wa kwanza kuzikutanisha timu hizo katika msimu huu, huku kila klabu ikiwa katika hali nzuri hivi sasa baada ya Simba kufanikiwa kuchukua ubingwa wa ligi na kombe la shirikisho huku Yanga ikirejea katika ubora baada ya kupitia misukosuko mbalimbali ikiwemo ya ukata wa fedha na kuondokewa kwa viongozi wake muhimu.
Simba na Yanga zimekutana mara 85 mpaka sasa katika ligi kuu Tanzania bara tangu ilipoanzishwa mwaka 1965, Yanga inaongoza kwa kushinda mara nyingi mtanange huo, ikiifunga Simba mara 31 huku Simba ikishinda mara 25 na kwenda sare mara 29.