Thursday , 28th Apr , 2016

Kocha wa Azam FC Stewart Hall na Daktari wa timu ya Coastal Union Mganga Kitambi wanatarajiwa kujadiliwa katika Kikao cha Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka nchini (TFF) Jumapili ya Mei Mosi mwaka huu.

Kamati hiyo ya Nidhamu itapitia mashauri mbalimbali yaliyowasilishwa ambapo mbali Stewart pamoja na Kitambi pia wapo wachezaji 15 ambao John Bocco, Shomari Kapombe, Aishi Manula na Kipre Tchetche wote wa Azam FC, Amissi Tambwe na Donald Ngoma wote wa Yanga SC, Paulo Jinga, Zephlyn Laurian na Idrisa Mohamed wote kutoka JKT Rwamkoma FC.

Wengine ni Ismail Nkulo, Said Juma, Idd Selaman na Edward Amos kutoka Polisi Dodoma, Herry Chibakasa kutoka Friends Rangers na Abel Katunda kutoka Transit Camp.