Thursday , 12th Nov , 2015

Mwakilishi wa Tanzania katika mashindano ya Afrika ya Mpira wa wavu wa ufukweni anatarajiwa kupatikana Desemba mwaka huu jijini Dar es salaam.

Katibu mkuu wa Chama cha Mpira wa Wavu wa Ufukweni TAVA Allen Alex amesema, wanatarajia kufanya mashindano ya taifa Desemba tisa mpaka 13 kwa ajili ya kupata mwakilishi wa kuwakilisha nchi katika mashindano hayo yatakayofanyika mwezi Machi mwakani nchini Misri.

Allen amesema, mashindano hayo yatashirikisha timu 18 za mikoa wanachama wa TAVA ambapo kabla ya kufanyika mashindano hayo utafanyika mkutano mkuu wa kuipitisha mikoa mingine mitano ambayo imeomba uanachama wa TAVA.

Allen amesema, mikoa mipya inatakiwa kuendelea kuomba uanachama na namna ya kuandaa katiba.