Wednesday , 24th Sep , 2014

Chama cha waandishi wa habari za michezo nchini TASWA kimeandaa tuzo za wanamichezo bora wa mwaka zinazotarajiwa kufanyika Desemba mwaka huu.

Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto

Akizungumza jijini Dar es salaam,Mwenyekiti wa TASWA Juma Pinto,amesema jinsi ya kuwapata wanamichezo hao vyama vya michezo mbalimbali hapa nchini vimetakiwa kutuma majina matatu ya wanamichezo ili kuweza kuchagua mwanamichezo atakayekuwa bora.

Pinto amesema wadhamini mbalimbali wanatakiwa kujitokeza ili kuweza kufanikisha tuzo hizo.