Friday , 26th Jun , 2015

Nchi wenyeji wa mashindano ya Taifa ya wazi ya mchezo wa Tenisi, Tanzania imetolewa katika hatua ya nusu fainali katika mashindano hayo yanayotarajiwa kumalizika hapo kesho katika uwanja wa Gymkhana jijini Dar es salaam.

Akizungumza na East Africa Radio, mratibu wa mashindano hayo, Salum Mvita amesema, watanzania walifanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali ambapo waliweza kutolewa katika hatua hiyo huku hatua ya fainali ikiwakutanisha Edgar Kazembe kutoka Zambia na David Olinga wa Uganda kwa upande wa wanaume huku kwa wanawake ikiwakutanisha Shufaa Changawa na Evelyne Otula wote wa Kenya.

Mvita amesema, kiwango kilikuwa kizuri kwa upande wa watanzania kwani mpaka kufikia hatua ya nusu fainali wamejitahidi na hiyo imetokana na watanzania wengi kuwa wachezaji wa nje ya nchi hivyo waliofika walicheza kwa kushindana zaidi na hayo ni sehemu ya matokeo.