Wednesday , 23rd Nov , 2016

Tottenham imetolewa kwenye Michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya, baada ya kuchapwa na Monaco mabao 2-1 katika Uwanja wa Stade Louis II, mjini Monaco.

 

Bao la mapema la mkwaju wa kichwa la Djibril Sidibe, lilimfikishia mchezaji huyo bao la tatu katika michezo mitano, lakini Spurs walisawazisha kupitia penalti ya Harry Kane kabla ya sekunde 39 baadaye Monaco kupata bao la pili kupitia Thomas Lemar.

Ushindi huo unaivusha Monaco kwenye hatua ya 16 bora ya ligi ya mabingwa Ulaya, kama vinara wa kundi E, juu ya Bayer Leverkusen, waliotoka  1-1 na CSKA Moscow.

Nao, mabingwa wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza Leicester City, imetinga hatua ya 16, bora baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Club Brugge katika Uwanja wa nyumbani King Power.