Katika mchezo huo wa raundi ya 17, Singida United walifanikiwa kufunga bao la kwanza dakika ya 45 kupitia kwa Shafik Batambuze kabla ya Mbao FC kusawazisha kupitia kwa Habib Kiyombo dakika ya 51.
Singida United walijihakikishia ushindi dakika ya 58 kupitia bao la Deus Kaseke ambalo limewapa alama tatu muhimu na kuwafikia Azam FC kwa alama 33.
Azam FC wamepoteza mechi yao ya raundi ya 17 dhidi ya Simba hivyo kubaki na alama 33 katika nafasi ya tatu wakilingana na Singida United.
