
Ikiwa ni sehemu ya maboresho na kuziba nafasi zilizoachwa na wachezaji walioondoka ndani ya Singida United, timu hiyo imemsainisha Mpepo mkataba wa miaka miwili.
Usajili wa Singida United ni sehemu ya mapendekezo ya kocha mpya wa timu hiyo Hemed Morocco, aliyechukua mikoba ya Hans Van Pluijm ambaye amejiunga na Azam, FC baada ya kuifundisha timu hiyo kwa msimu mmoja.
Usajili wa Mpepo ni wazi kuwa anakuja kuchukua nafasi ya mshambuliaji kutoka Zimbabwe Tafadzwa Kutinyu ambaye alikuwa tegemeo kwa Singida United msimu uliopita lakini ameungana na kocha Hans ndani ya Azam FC.
Msimu uliopita Singida United ilimaliza katika nafasi ya tano ikiwa na alama 44 huku Tanzania Prison ikimaliza katika nafasi ya nne ikiwa na alama 48.