Makamu wa Rais wa klabu ya Simba, Geofrey Nyange 'Kaburu'
Kaburu amefafanua jambo hilo baada ya kuenea uvumi kuwa timu hiyo iligoma kwenda kupokea tuzo zao kama walivyofanya wachezaji wengine waliotajwa jana katika hafla iliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam.
"Sisi tupo Dodoma tunajiandaa na maandalizi yetu ya mwisho ya fainali za FA dhidi ya wapinzani wetu Mbao FC na hatujaweza kutuma mwakilishi yeyote katika hafla hiyo kutokana na viongozi wote tupo huku....Tukirudi ndiyo tutajua cha kufanya kama tukienda kuchukua tuzo hizo tutawaambia lakini sasa hivi ni mapema kulisema hilo". Alisema Kaburu
Pamoja na hayo, Kaburu amesema timu yake imejiandaa vizuri katika fainali hiyo ili waweze kuchukua ubingwa na kuweza kuwakalisha nchi katika mashindano ya kimataifa.

