Kikosi cha Simba kimeondoka jijini Dar es Salaam leo alfajiri kwenda mkoani Shinyanga kwa ajili ya mechi yake ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagare Sugar.
Simba wameondoka na basi lao wakiwa na kikosi kamili kasoro mshambuliaji Paul Kiongera ambaye ni majeruhi na amerejea kwao Kenya kujiuguza.
Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano ya klabu ya Simba,Haji Manara amesema"Baada ya kazi moja, inafuata nyingine. Tumeanza safari ya kwenda Shinyanga, tunaomba dua zenu,".Alisema Manara.
Mechi hiyo itapigwa kesho kutwa Jumamosi kwa kuwa Kagera Sugar imeamua kuuhama Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora na kurejea Shinyanga. Hii inatokana na Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba kuwa kwenye matengenezo makubwa.
Simba inakwenda Shinyanga baada ya kuwa imetoa kipigo cha mabao 5-1 kwa Mgambo Shooting ya Tanga, jana uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.



