Sunday , 25th May , 2014

zoezi la kuwahoji walioweka na kuwekewa pingamizi limeanza hii leo kwa kamati ya uchaguzi ya klabu ya Simba iliyochini ya mwenyekiti wake Dr. Damas Ndumbaro ambaye amewataka wanachama wa klabu hiyo kuwa makini na kanuni za uchaguzi.

Baadhi ya wanachama wa Simba wakiwa katika moja ya mikutano ya klabu hiyo

Mchakato wa uchaguzi wa klabu ya Simba ambao unaendelea hivi sasa mara baada ya zoezi la kupokea mapingamizi, hii leo kamati ya uchaguzi ya klabu hiyo imekutana tayari kwa uanza kusikiliza mapingamizi hayo

Mwenyekiti wa kamati hiyo Dr. Damas Ndumbaro amesema kikao hicho kitawahusisha walioweka na kuwekea pingamizi pekee na kinafanyika kwa siku mbili kuanzia hii leo

Ndumbalo amewataka wanachama wa kabu hiyo kuwapa nafasi wafanye kazi na majibu ya kikao hicho watayatoa may 27 mwaka huu tayari kwa zoezi la usaili

Aidha Ndumbaro amesema kila aliyeweka na kuwekewa pingamizi ni lazima aje na vielelezo vya kutetea hoja yake.