
Klabu ya soka ya Simba hii leo imefanya mkutano wa wanachama wake katika ukumbi wa bwalo la maofisa wa polisi oysterbay jijini Dar es salaam mkutano ambao ulikua na ajenda moja tu kwa ajili ya kuifanyia marekebisho Katiba yao
Baada ya majadiliano marefu hatimaye mabadiliko ya katiba hiyo yalifanywa kwac maridhiano ya wanachama wengi katika mkutano huo ambao uliongozwa na mwenyekiti wa klabu hiyo Ismail Aden Rage ambaye aliwapongeza wanachama wote kwakufanikisha zoezi hilo kwa amani na utulivu mkubwa
Aidha Rage kwaniaba ya wanasimba wote amempongeza na kumshukuru rais Jakaya Kikwete kwa msaada wake wa shilingi milioni 30 alizotoa kusaidia ujenzi wa uwanja wa timu hiyo.