Monday , 4th Jan , 2016

Serikali na wadau nchini wametakiwa kujitokeza kwa ajili ya kuisaidia timu ya taifa ya ngumi ya wanawake inayojiandaa kushiriki mashindano ya Olimpiki mwaka huu nchini Brazili.

Mjumbe wa maendeleo ya wanawake wa Shirikisho la Ngumi nchini BFT Aisha Voniatis amesema, kwa mwaka huu wameshindwa kushiriki mashindano mengi ya kuwania kufuzu mashindano ya Olimpiki hivyo kuwaweka katika kipindi kigumu wachezaji ambao wapo katika maandalizi ya michuano ya Olimpiki.

Aisha amesema, mabondia wa kike wanashindwa kufanya vizuri kutokana na kukosa watu wa kuwaunga mkono katika mashindano mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.