
Akizungumza na East Africa Radio, Kocha wa Mabondia wa Klabu ya Mabibo Damian Mkandawile amesema, wameamua kuanzisha mafunzo kwa mabondia mbalimbali ili kuweza kuwaepusha na mambo mbalimbali ikiwemo utumiaji wa madaya ya kulevya pamoja na wizi.
Mkandawile amesema, klabu hiyo mpaka sasa inavijana zaidi ya 20 lakini haina vifaa vya kutosha kwa ajili ya kuiwezesha kuendelea kuwa na vijana wengi watakaoweza kupokea mafunzo na kuweza kupanda ulingoni kwa ajili ya kuweza kupambana.
Mkandawile amesema, mwelekeo wa vijana hao katika kupokea mafunzo ni mzuri na anaamini wataweza kufanya vizuri hata katika mapambano mbalimbali ambayo yatakuwa yameandaliwa na kuweza kujiimarisha zaidi katika mchezo huo.