Wednesday , 20th Jan , 2016

Mabingwa watetezi wa mashindano ya wazi ya Australia Novak Djkovic na Serena Williams wamefuzu kuingia raundi ya tatu ya michuano hiyo inayoendelea huko Melbourne Park hii leo.

Mabingwa watetezi wa mashindano ya wazi ya Australia Novak Djkovic na Serena Williams wamefuzu kuingia raundi ya tatu ya michuano hiyo inayoendelea huko Melbourne Park hii leo.

Djkovic anayeshika namba moja kwa upande wa wanaume ametinga hatua hiyo kwa kumgalagaza Quentin Halys kwa seti 6-1 6-2 7-6 (7-3).

Naye Williams anayeshika namba moja kwa ubora wa tenesi dunani alimwondosha Hsieh Su-Wei kwa seti 6-1 6-2.

Wengine walioshinda hii leo ni pamoja na Roger Federer na Maria Sharapova, wakati bingwa mara mbili wa Wimbledon Petra Kvitova alistaajabishwa na kijana wa miaka 21 kutoka Australia Daria Gavrilova kwa 6-4 6-4 na kuaga safari.

Wakati huo huo Venus Williams amepigwa faini ya dola za kimarekani 5000 zaidi ya shilingi million 10 za kitanzania kwa kushindwa kutokea katika mkutano na waandishi wa habari baada ya mchezo wake wa jana ambao alipoteza.

Venus ambaye anakamata nafasi ya 10 akiwa na mataji 7 ya Grand Slam, alifungwa na muingereza Johanna Konta na kutupwa nje ya mashindano hayo.