Samuel Umtiti
Samuel Umtiti mwenye umri wa miaka 22 alifanya vizuri katika michuano ya Euro 2016 aliisaidia timu yake ya taifa ya Ufaransa kutinga fainali za michuano hiyo japo waliambulia kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Ureno.
Aidha, Samuel amesajiliwa na klabu hiyo kwa mkataba wa miaka mitano na atakuwa akicheza nafasi ya beki wa kushoto au beki wa kati.
Barcelona wenyewe wamethibitisha kukamilika kwa usahili huo jana baada ya kutangaza kumtaka mchezaji huyo toka mwezi Juni.



