Mbwana Ally Samatta.
KRC Genk imeshinda 1-0 baada ya Samatta kufunga bao hilo katika dakika ya 82 akiunganisha pasi safi ya Ruslan Malinovysky na kutoka na point tatu ugenini katika uwanja wa Stadion am Kehrweg.
Samatta ambaye amecheza kwa dakika zote 90, alionyesha uwezo mkubwa ikiwa ni pamoja na kuwapa wakati mgumu mabeki wa KAS Eupen kwani licha ya kuwa ugenini walimiliki mpira kwa asilimia 55 na wenyeji hao walimiliki mpira kwa asilimia 45.
Ushindi huo wa KRC Genk umeisongeza klabu hiyo hadi katika nafasi ya 8 ikiwa na pointi 31 katika msimamo wa Ligi Kuu Ubelgiji inayoshikisha timu 16, huku Klabu ya Brugge ikiendelea kuwa kinara wa Ligi Kuu Ubelgiji ikiwa na pointi 43.