Tuesday , 1st Sep , 2015

Shirikisho la soka nchini TFF limesema, walitarajia timu ya taifa ya Twiga Stars usiku wa jana ingeondoka kuelekea nchini Congo Brazzaville kwa ajili ya mashindano ya All African Games lakini imeshindikana kutokana na kuchelewa kwa tiketi.

Katibu Mkuu wa TFF, Celestine Mwesigw aamesema, kuna baadhi ya mambo hayajakamilika kwa ajili ya timu hiyo kuanza safari lakini wanatarajia leo au kesho timu hiyo kuanza safari kwa ajili ya maandalizi ya michuano hiyo.

Twiga Stars iliyochini ya Kocha wake Rogasian Kaijage inatarajia kuanza mechi yake ya kwanza ya kundi A September 06 mwaka huu dhidi ya Ivory Coast huku timu nyingine zilizo na Twiga Stars katika kundi hilo zikiwa ni wenyeji Congo Brazzaville na Nigeria.

Kundi B katika michuano hiyo kwa upande wa Timu ya wanawake ni timu za Cameroon, Afrika Kusini, Ghana, Egypt ambapo mshindi kwa kwanza na wa pili kwa kila kundi atafuzu hatua ya nusu fainali.