Saturday , 30th Jan , 2016

Timu ya Amavubi ya Rwanda imetupwa nje ya michuano ya CHAN katika hatua ya robo fainali baada ya kufungwa na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mabao 2-1.

Timu ya taifa ya Rwanda Amavubi ambao ni wenyeji wa michuano ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza katika ligi za nchi zao barani Afrika CHAN, imevurumishwa nje ya michuano hiyo katika hatua ya robo fainali baada ya kufungwa na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mabao 2-1.

Magoli ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yamefungwa na Gikanji dakika ya 11 na Padou Bompunga dakika ya 113 huku la Amavubi likifungwa na Jean-Claude Iranzi katika mchezo uliokwenda kwa dakika 120 baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya bao 1-1.

Katika robo fainali ya pili, Ivory Coast imeungana na DRC kutinga nusu fainali baada ya kuichapa Cameroon mabao 3-0.
Mabao yote ya Cameroon yamepatikana katika muda wa dakika 30 za zoada baada ya timu hizo kutofungana katika dakika zote 90.

Mabao ya Cameroon yamefungwa na Boua dakika ya 95, Atcho dakika ya 102 na Serge Yao Nguessan dakika ya 112.
Robo fainali ya michuano hiyo itaendelea kesho kwa michezo miwili ambapo Tunisia itakabiliana na Mali saa 10:00 jioni huku Zambia ikikabiliana na Guinea saa 1:00 jioni.