Nyambui ambaye kwasasa ni kocha mkuu wa Timu ya Taifa ya Riadha ya Brunei amesema, wanariadha hao hawawezi kupata medali hadi pale Taifa kwa ujumla wake likiamua kuwa limepania kutafuta medali katika michuano hiyo.
Nyambui amesema, Olimpiki sio mashindano ya majaribio hivyo washiriki wanatakiwa waandaliwe mazingira maalumu na wafundishwe na makocha maalumu kwa muda wote uliobakia jambo ambalo haliwezi kufanywa na RT pekee bali Serikali inatakiwa kuwajibika kwa kiasi kikubwa kutekeleza jukumu hilo ndipo wataweza kupata medali.

