Tuesday , 3rd Jan , 2017

Kocha wa man City Pep Guardiola amesema kuwa klabu hiyo inawezakuwa klabu yake ya mwisho kuifundisha soka baada ya kukasirishwa na maamuzi ya mwamuzi wa mchezo wa jana dhidi ya Bournemouth.

Pep Guardiola

City, ilipata ushindi wa mabao 2-1, kwenye mchezo huo, uliochezwa uwanja wa nyumbani wa Etihad, na kushuhudiwa na kiungo wake mkabaji Fernandinho akipewa kadi nyekundu.

Guardiola, aliyesaini Man City kwa kandarasi ya miaka 3 na hadi sasa akiwa ndiyo kwanza ana miezi 6 na klabu hiyo, amesema asingependa kufundisha mpira hadi umri wa miaka 65, hivyo klabu hiyo ya Man City ni ya mwisho kwake kufundisha.

''Nitakuwa hapa Manchester kwa misimu ama mitatu labda na zaidi, sitakaa kwenye benchi mpaka miaka 60 au 65. Nafikiri mchakato wa kuanza kusema kwaheri umekaribia'' Alisema Guardiola.

Muispania huyo amewahi kuifundisha klabu ya Barcelona kwa mafanikio makubwa kisha Bayern Munich kabla ya kuchukua nafasi ya Manuel Pellegrini Man city.

Mtindo wake wa kuachana na soka unaweza kufanana na ule wa kocha wa kitanzania Jamhuri Kihwelo 'Julio' aliyestaafu kufundisha soka kwa madai ya kuchoshwa na waamuzi.