Oscar Pistorius (pichani) akionekana mwenye majonzi mahakamani.
Mwanariadha huyo alipatikana na hatia ya kumuua mpenzi wake mwaka 2013 na kuhukumiwa kwa kosa la kuuwa bila ya kukusudia lakini ilikatwa rufaa iliyopelekea kutenguliwa kwa hukumu hiyo.
Katika tukio la aina yake mwezi uliopita wakati wa kusikilizwa kwa shauri hilo mwanariadha huyo alishauriwa na timu ya wanasheria wanaomtetea kuvua miguu ya bandia na kutembea kwenye chumba cha mahakama bila miguu hiyo, Ili kutoa ushawishi kwa jaji kuamini kuwa hakuwa na uwezo wa kufanya mauaji hayo.
Pistorius tayari ameshatumikia kifungo cha takribani miezi tisa jela katika kosa la awali wakati alipopatikana na hatia ya kuua bila kukusudia mwaka 2013, na alikuwa anaendelea na kifungo hicho nyumbani, kabla ya hukumu ya hii leo.
Kwa sasa kifungo chake kimeongezeka baada ya upande wa serikali kushinda rufaa hiyo ambapo kosa lake lilibadilika na kuwa kosa la kuua kwa kukusudia.

