
Katika taarifa yake, Msemaji wa klabu hiyo Idrissa Bandari amesema, kikosi chao kinaendelea vizuri na mazoezi na vijana wote wanaonesha kujituma hivyo wanaamini kuwa mazoezi hayo watafanya vizuri kwenye Ligi.
Bandari amesema, wanampango wa kucheza mechi za kirafiki ili kukinoa zaidi kikosi chao ambapo wamepanga kuanza na kucheza na Mtibwa Sugar kama mipango yao itakaa sawa.