Akizungumza na East Africa Radio, Kocha wa Kocha wa Timu ya Taifa ya Kriketi Kharil Remtullah amesema timu inaendelea na mazoezi ambapo hivi sasa wapo katika hatua ya mwisho ambayo ni ya mikimbio pamoja na masharti yote ya mchezo.
Kharil amesema, timu kutoka nchi shiriki za michuano nchi shiriki za michuano hiyo zinatarajiwa kuwasili nchini kuanzia Fabruari 12 mwaka huu ambapo katika kikosi chake cha vijana 14 ana majeruhi wawili ambao ni majeruhi lakini wanaendelea na matibabu huku wakiendelea na mazoezi madogo madogo kwa ajili ya kujiweka sawa kiafya.