
Kikosi cha Simba na Mwinyi Zahera
Zahera ameyasema hayo kwenye mahojiano maalum na www.eatv.tv ambapo ameweka wazi kuwa yeye ni kocha na anapopata nafasi timu yoyote lazima akubali kufanya kazi.
''Mpira ni kitu cha ajabu sana, kwasasa Yanga tunashinda na mashabiki wananipenda wanasema kocha mzuri lakini tukifungwa mechi 5 mfululizo watanikataa na kunifukuza, sasa Simba wakija nitakaa vipi wakati mimi ni kocha'', amesema Zahera.
Aidha kocha huyo raia wa Congo aliongeza kuwa anafanya kazi Yanga kwa mapenzi yake yote lakini ukifika muda timu haipati matokeo ni ngumu viongozi kumvumilia lazima watamuondoa.
Zahera ameiwezesha Yanga kuongoza ligi kuu soka Tanzania bara ikiwa na alama 50 kwenye mechi 18.
Zaidi sikiliza mahojiano hapo chini.