
Wachezaji wa Taifa Stars (kushoto) na Mwinyi Zahera (kulia)
Akiongea kwa simu na www.eatv.tv kutoka Kinshasa DR Congo, Zahera amesema jana ilikuwa ni siku ya furaha sana, haswa baada ya kushinda mchezo wao na Liberia na kufuzu AFCON 2019, kisha kuishuhudia Stars ikifuzu pia kwa kuifunga Uganda.
''Baada tu ya mchezo wetu nikamsubiri Rais Felix Tshisekedi, alipokuja kwenye vyumba vya kubadilishia nguo kutupongeza lakini alipomaliza tu mimi nikakimbia hotelini kuingalia mechi ya Taifa Stars na nikakuta wanaongoza kwa bao 1-0 hivyo nikaona mabao mawili'', amesema.
Zahera pia ameeleza kuwa Taifa Stars walicheza mpira mzuri sana na kwa dakika chache tu, aliamini watashinda kwa mabao matatu na kweli wakafunga la pili kwa penati ambapo alishangilia kiasi cha wenzake kumshangaa sana haswa lilipoongezwa bao la tatu.
Zaidi msikilze hapa akifafanua zaidi.