
Bao pekee la Mwadui FC inayofundishwa na Jamhuri Mussa Kihwelo ‘Julio’, limefungwa na Salum Iyee dakika ya 85 akimalizia pasi maridadi ya kiungo Maregesi Mwangwa.
Mwadui imemaliza na pointi sita baada ya awali kuifunga Toto African pia 1-0 ambapo Toto imemaliza nafasi ya pili kwa pointi zake tatu baada ya kuifunga Kagera Sugar 2-0.
Stand United ya Shinyanga iliondolewa kwenye mashindano baada ya mechi moja tu na Mwadui ikifungwa 4-0, kufuatia kuchezesha wachzaji wa timu ya vijana, jambo ambalo lilikuwa kinyume cha kanuni ambapo matokeo ya Stand United na Mwadui yalifutwa na michuano ikabaki na timu tatu hatimaye Mwadui wameibuka mabingwa.